Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 49:13-20

Zaburi 49:13-20 BHN

Hayo ndiyo yawapatao wanaojiamini kipumbavu, ndio mwisho wa wale wanaojivunia mali zao. Wataongozwa kama kondoo hadi kuzimu, kifo kitakuwa mchungaji wao. Watashuka moja kwa moja kaburini. Miili yao itaozea huko, Kuzimu kutakuwa makao yao. Lakini Mungu ataniokoa na kuzimu. Atanisalimisha kutoka huko. Usihangaike ukiona mtu anatajirika, wala mali yake ikiongezeka zaidi na zaidi. Maana atakapokufa hatachukua chochote, mali yake haitashuka huko chini pamoja naye. Ajapojikuza katika maisha haya, na kusifiwa kwa sababu ya kufanikiwa, atajiunga na wazee waliomtangulia kufa, ambao hawawezi kuona tena mwanga. Binadamu hatadumu milele katika fahari yake, atakufa tu kama mnyama.

Soma Zaburi 49

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 49:13-20