Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 49:13-20

Zaburi 49:13-20 SRUV

Hiyo ndiyo njia yao, ujinga wao, Nao walioko baada yao huyaridhia maneno yao. Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na kifo kitakuwa mchungaji wao; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Miili yao itaoza, kao lao ni kuzimu. Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanipokea. Usiogope mtu atakapopata utajiri, Na fahari ya nyumba yake itakapoongezeka. Maana atakapokufa hatachukua chochote; Utukufu wake hautashuka ukimfuata. Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai, Na watu watakusifu ukijitendea mema, Atakwenda kwenye kizazi cha baba zake Hawataona nuru hata milele. Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili, Amefanana na wanyama wapoteao.

Soma Zaburi 49

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 49:13-20