Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 49:13-20

Zab 49:13-20 SUV

Hiyo ndiyo njia yao, ujinga wao, Nao walioko baada yao huyaridhia maneno yao. Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na mauti itawachunga; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Umbo lao litachakaa, kao lao ni kuzimu. Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha. Usiogope mtu atakapopata utajiri, Na fahari ya nyumba yake itakapozidi. Maana atakapokufa hatachukua cho chote; Utukufu wake hautashuka ukimfuata. Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai, Na watu watakusifu ukijitendea mema, Atakwenda kwenye kizazi cha baba zake Hawataona nuru hata milele. Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili, Amefanana na wanyama wapoteao.

Soma Zab 49

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 49:13-20