Zaburi 31:6-10
Zaburi 31:6-10 BHN
Wawachukia wanaoabudu sanamu batili; lakini mimi nakutumainia wewe, ee Mwenyezi-Mungu. Nitashangilia na kufurahia fadhili zako, maana wewe waiona dhiki yangu, wajua na taabu ya nafsi yangu. Wewe hukuniacha nitiwe mikononi mwa maadui zangu; umenisimamisha mahali pa usalama. Unionee huruma, ee Mwenyezi-Mungu, niko taabuni; macho yangu yamechoka kwa huzuni, nimeishiwa nguvu mwilini na rohoni. Maisha yangu yamekwisha kwa majonzi; naam, miaka yangu kwa kulalamika. Nguvu zangu zimeniishia kwa kutaabika; hata mifupa yangu imekauka.