Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 31:6-10

Zab 31:6-10 SUV

Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo; Bali mimi namtumaini BWANA. Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako, Kwa kuwa umeyaona mateso yangu. Umeijua nafsi yangu taabuni, Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi. Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki, Jicho langu limenyauka kwa masumbufu, Naam, mwili wangu na nafsi yangu. Maana maisha yangu yamekoma kwa huzuni, Na miaka yangu kwa kuugua. Nguvu zangu zinatetemeka kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imekauka.

Soma Zab 31

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 31:6-10