Zaburi 31:6-10
Zaburi 31:6-10 NEN
Ninawachukia wale wanaongʼangʼania sanamu batili; mimi ninamtumaini BWANA. Nitafurahia na kushangilia upendo wako, kwa kuwa uliona mateso yangu na ulijua maumivu ya nafsi yangu. Hukunikabidhi kwa adui yangu bali umeiweka miguu yangu mahali penye nafasi. Ee BWANA unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida; macho yangu yanafifia kwa huzuni, nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko. Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, na mifupa yangu inachakaa.