Zaburi 25:15-18
Zaburi 25:15-18 BHN
Namwangalia Mwenyezi-Mungu daima; yeye atainasua miguu yangu mtegoni. Unielekee, ee Mungu, unionee huruma, maana mimi ni mpweke na mnyonge. Uniondolee mahangaiko ya moyoni mwangu; unitoe katika mashaka yangu. Uangalie mateso yangu na dhiki yangu; unisamehe dhambi zangu zote.