Zaburi 25:15-18
Zaburi 25:15-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Macho yangu humwelekea BWANA daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu. Uniangalie na kunifadhili, Maana mimi ni mkiwa na mteswa. Katika shida za moyo wangu unifanyie nafasi, Na kunitoa katika dhiki zangu. Utazame teso langu na taabu yangu; Unisamehe dhambi zangu zote.
Zaburi 25:15-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Namwangalia Mwenyezi-Mungu daima; yeye atainasua miguu yangu mtegoni. Unielekee, ee Mungu, unionee huruma, maana mimi ni mpweke na mnyonge. Uniondolee mahangaiko ya moyoni mwangu; unitoe katika mashaka yangu. Uangalie mateso yangu na dhiki yangu; unisamehe dhambi zangu zote.
Zaburi 25:15-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Macho yangu humwelekea BWANA daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu. Uniangalie na kunifadhili, Maana mimi ni mkiwa na mteswa. Uniondolee shida za moyo wangu, Na kunitoa katika dhiki zangu. Utazame mateso yangu na taabu yangu; Unisamehe dhambi zangu zote.
Zaburi 25:15-18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Macho yangu humwelekea BWANA daima, kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa miguu yangu kutoka mtego. Nigeukie na unihurumie, kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka. Shida za moyo wangu zimeongezeka, niokoe katika dhiki yangu. Uangalie mateso na shida zangu na uniondolee dhambi zangu zote.