Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 25:11-22

Zaburi 25:11-22 BHN

Kwa ajili ya jina lako, ee Mwenyezi-Mungu, unisamehe kosa langu kwani ni kubwa. Kila mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi-Mungu atamfunza njia ya kufuata. Mtu wa namna hiyo atafanikiwa daima, na wazawa wake watamiliki nchi. Mwenyezi-Mungu ni rafiki ya wale wamchao; yeye huwajulisha hao agano lake. Namwangalia Mwenyezi-Mungu daima; yeye atainasua miguu yangu mtegoni. Unielekee, ee Mungu, unionee huruma, maana mimi ni mpweke na mnyonge. Uniondolee mahangaiko ya moyoni mwangu; unitoe katika mashaka yangu. Uangalie mateso yangu na dhiki yangu; unisamehe dhambi zangu zote. Angalia jinsi walivyo wengi maadui zangu; ona jinsi wanavyonichukia kwa ukatili. Uyalinde maisha yangu, uniokoe; nakimbilia usalama kwako, usikubali niaibike. Wema na uadilifu vinihifadhi, maana ninakutumainia wewe. Ee Mungu, uwaokoe watu wako, Israeli; uwaokoe katika taabu zao zote.

Soma Zaburi 25