Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 141:1-10

Zaburi 141:1-10 BHN

Nakuita, ee Mwenyezi-Mungu, uje haraka kunisaidia! Uisikilize sauti yangu wakati ninapokuita! Sala yangu uipokee kama ubani; niinuapo mikono yangu kwako unikubali kama tambiko ya jioni. Ee Mwenyezi-Mungu ukilinde kinywa changu, uweke ulinzi mlangoni mwa mdomo wangu. Unikinge nisielekee kufanya mabaya, nisijishughulishe na matendo maovu; nisijiunge na watu watendao mabaya, wala nisishiriki kamwe karamu zao. Afadhali mtu mwema anipige kunionya; lakini sikubali kamwe kusifiwa na wabaya, maana nasali daima dhidi ya maovu yao. Wakuu wao watakapopondwa miambani, ndipo watatambua maneno yangu yalikuwa sawa. Mifupa yao itatawanywa mdomoni pa Kuzimu kama kuni zilizopasuliwa vipandevipande! Bali mimi nakutegemea, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu; ninakimbilia usalama kwako, usiniache hatarini. Unikinge na mitego waliyonitegea, uniepushe na matanzi ya hao watu waovu. Waovu wanaswe katika mitego yao wenyewe, wakati mimi najiendea zangu salama.

Soma Zaburi 141