Zaburi 141:1-10
Zaburi 141:1-10 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ee Mwenyezi Mungu, ninakuita, njoo kwangu hima. Sikia sauti yangu ninapokuita. Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba; kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni. Ee Mwenyezi Mungu, weka mlinzi kinywani mwangu, weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu. Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya, nisije nikashiriki katika matendo maovu pamoja na watu watendao mabaya, wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa. Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma; na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu. Kichwa changu hakitalikataa. Hata hivyo, maombi yangu daima ni kinyume cha watenda maovu. Watawala wao watatupwa chini kutoka majabali, waovu watajifunza kwamba maneno yangu yalikuwa kweli. Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi, ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.” Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, ndani yako nimekimbilia, usiniache nife. Niepushe na mitego waliyonitegea, kutokana na mitego iliyotegwa na watenda maovu. Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe, wakati mimi ninapita salama.
Zaburi 141:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Nakuita, ee Mwenyezi-Mungu, uje haraka kunisaidia! Uisikilize sauti yangu wakati ninapokuita! Sala yangu uipokee kama ubani; niinuapo mikono yangu kwako unikubali kama tambiko ya jioni. Ee Mwenyezi-Mungu ukilinde kinywa changu, uweke ulinzi mlangoni mwa mdomo wangu. Unikinge nisielekee kufanya mabaya, nisijishughulishe na matendo maovu; nisijiunge na watu watendao mabaya, wala nisishiriki kamwe karamu zao. Afadhali mtu mwema anipige kunionya; lakini sikubali kamwe kusifiwa na wabaya, maana nasali daima dhidi ya maovu yao. Wakuu wao watakapopondwa miambani, ndipo watatambua maneno yangu yalikuwa sawa. Mifupa yao itatawanywa mdomoni pa Kuzimu kama kuni zilizopasuliwa vipandevipande! Bali mimi nakutegemea, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu; ninakimbilia usalama kwako, usiniache hatarini. Unikinge na mitego waliyonitegea, uniepushe na matanzi ya hao watu waovu. Waovu wanaswe katika mitego yao wenyewe, wakati mimi najiendea zangu salama.
Zaburi 141:1-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, nimekuita, unijie hima, Uisikie sauti yangu nikuitapo. Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni. Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu. Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa. Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao. Wakuu wao wakiangushwa kando ya genge, Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu. Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu. Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana, Nimekukimbilia Wewe, usiniache bila kinga. Unilinde kutoka kwa mtego walionitegea, Na kutoka kwa matanzi ya watendao maovu. Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Wakati ninapopita salama.
Zaburi 141:1-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, nimekuita, unijie hima, Uisikie sauti yangu nikuitapo. Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni. Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu. Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa. Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao. Makadhi wao wakiangushwa kando ya genge, Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu. Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu. Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana, Nimekukimbilia Wewe, usiniache nafsi yangu. Unilinde na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu. Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Pindi mimi ninapopita salama.