Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 125:1-5

Zaburi 125:1-5 BHN

Wanaomtegemea Mwenyezi-Mungu, wako kama mlima Siyoni, ambao hautikisiki bali wabaki imara daima. Kama Yerusalemu inavyozungukwa na milima, ndivyo Mwenyezi-Mungu awazungukavyo watu wake, tangu sasa na hata milele. Waovu hawataendelea kutawala nchi ya waadilifu; wasije waadilifu nao wakafanya maovu. Ee Mwenyezi-Mungu, uwe mwema kwa watu wema, kwa wale wanaozitii amri zako. Lakini wanaogeuka na kufuata njia zao mbaya uwakumbe pamoja na watenda maovu. Amani iwe na Israeli!

Soma Zaburi 125

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 125:1-5