Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 125:1-5

Zaburi 125:1-5 SRUV

Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautikisiki, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya nchi ya wenye haki; Ili wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu. Ee BWANA, uwatendee mema walio wema, Nao walio wanyofu wa moyo. Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.

Soma Zaburi 125

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 125:1-5