Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 125:1-5

Zab 125:1-5 SUV

Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu. Ee BWANA, uwatendee mema walio wema, Nao walio wanyofu wa moyo. Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli.

Soma Zab 125

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 125:1-5