Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 119:65-77

Zaburi 119:65-77 BHN

Umenitendea vema mimi mtumishi wako, kama ulivyoahidi, ee Mwenyezi-Mungu. Unifundishe akili na maarifa, maana nina imani sana na amri zako. Kabla ya kuniadhibu nilikuwa nikikosea, lakini sasa nashika neno lako. Wewe ni mwema na mfadhili; unifundishe masharti yako. Wenye kiburi wanasema uongo juu yangu, lakini mimi nashika kanuni zako kwa moyo wote. Mioyo yao imejaa upumbavu, lakini mimi nafurahia sheria yako. Nimefaidika kutokana na taabu yangu, maana imenifanya nijifunze masharti yako. Sheria uliyoweka ni bora kwangu, kuliko mali zote za dunia. Mikono yako iliniumba na kuniunda; unijalie akili nijifunze amri zako. Wakuchao wataniona na kufurahi, maana tumaini langu liko katika neno lako. Najua hukumu zako ni adili, ee Mwenyezi-Mungu, na kwamba umeniadhibu kwani wewe ni mwaminifu. Fadhili zako na zinipe faraja, kama ulivyoniahidi mimi mtumishi wako. Unionee huruma nipate kuishi, maana sheria yako ni furaha yangu.

Soma Zaburi 119

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha