Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 119:65-77

Zaburi 119:65-77 SRUV

Umemtendea mtumishi wako mema, Ee BWANA, sawasawa na neno lako. Unifundishe akili na maarifa, Maana nimeyaamini maagizo yako. Kabla sijateswa mimi nilipotea, Lakini sasa nimelitii neno lako. Wewe U mwema na mtenda mema, Unifundishe amri zako. Wenye kiburi wamenizulia uongo, Lakini kwa moyo wangu wote nitayashika mausia yako. Mioyo yao imenenepa kama shahamu, Lakini mimi nimeifurahia sheria yako. Ilikuwa vema kwangu kuwa niliteswa, Nipate kujifunza amri zako. Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu, Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha. Mikono yako iliniumba na kunidhibiti, Unifahamishe nikajifunze amri zako. Wakuchao na wanione na kufurahi, Kwa sababu nimelitumainia neno lako. Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee BWANA, na kwa uaminifu umenitesa. Nakuomba, fadhili zako ziwe faraja kwangu, Kulingana na ahadi yako kwa mtumishi wako. Rehema zako zinijie nipate kuishi, Maana sheria yako ni furaha yangu.

Soma Zaburi 119