Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 119:65-77

Zab 119:65-77 SUV

Umemtendea mema mtumishi wako, Ee BWANA, sawasawa na neno lako. Unifundishe akili na maarifa, Maana nimeyaamini maagizo yako. Kabla sijateswa mimi nalipotea, Lakini sasa nimelitii neno lako. Wewe U mwema na mtenda mema, Unifundishe amri zako. Wenye kiburi wamenizulia uongo, Kwa moyo wangu wote nitayashika mausia yako. Mioyo yao imenenepa kama shahamu, Mimi nimeifurahia sheria yako. Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa, Nipate kujifunza amri zako. Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu, Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha. Mikono yako ilinifanya ikanitengeneza, Unifahamishe nikajifunze maagizo yako. Wakuchao na wanione na kufurahi, Kwa sababu nimelingojea neno lako. Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee BWANA, na kwa uaminifu umenitesa. Nakuomba, fadhili zako ziwe faraja kwangu, Sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako. Rehema zako zinijie nipate kuishi, Maana sheria yako ni furaha yangu.

Soma Zab 119

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha