Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 118:1-7

Zaburi 118:1-7 BHN

Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake zadumu milele. Watu wa Israeli na waseme: “Fadhili zake zadumu milele.” Wazawa wa Aroni na waseme: “Fadhili zake zadumu milele.” Wote wamchao Mwenyezi-Mungu na waseme: “Fadhili zake zadumu milele.” Katika taabu yangu nilimwomba Mwenyezi-Mungu, naye akanisikia na kuniweka huru. Mwenyezi-Mungu yuko nami, siogopi kitu; binadamu ataweza kunifanya nini? Mwenyezi-Mungu yuko nami, kunisaidia; nami nitawaona maadui zangu wameshindwa.

Soma Zaburi 118