Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 118:1-7

Zaburi 118:1-7 NEN

Mshukuruni BWANA, kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. Israeli na aseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.” Nyumba ya Aroni na iseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.” Wote wamchao BWANA na waseme sasa: “Upendo wake wadumu milele.” Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia BWANA, naye akanijibu kwa kuniweka huru. BWANA yuko pamoja nami, sitaogopa. Mwanadamu anaweza kunitenda nini? BWANA yuko pamoja nami, yeye ni msaidizi wangu. Nitawatazama adui zangu wakiwa wameshindwa.