Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 118:1-7

Zaburi 118:1-7 SRUV

Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele. Israeli na aseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele. Mlango wa Haruni na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele. Wamchao BWANA na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele. Katika shida yangu nilimwita BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi. BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wakiwa wameshindwa.

Soma Zaburi 118