Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 26:17-21

Methali 26:17-21 BHN

Ajiingizaye katika ugomvi usiomhusu, ni kama mtu amshikaye masikio mbwa anayepita. Kama mwendawazimu achezeavyo mienge, au mishale ya kifo, ndivyo alivyo mtu ampotoshaye jirani, kisha aseme, “Nilikuwa natania tu!” Bila kuni, moto huzimika; bila mchochezi, ugomvi humalizika. Kama vile makaa au kuni huchochea moto, ndivyo mgomvi achocheavyo ugomvi.

Soma Methali 26