Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 26:17-21

Mithali 26:17-21 NEN

Kama yeye amkamataye mbwa kwa masikio, ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu. Kama mtu mwendawazimu atupaye vijinga vya moto au mishale ya kufisha, ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema, “Nilikuwa nikifanya mzaha tu!” Bila kuni moto huzimika; pasipo uchongezi ugomvi humalizika. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi.