Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 26:17-21

Mithali 26:17-21 SRUV

Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake; Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake. Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, Na mishale, na mauti; Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu? Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, Na kama kuni juu ya moto; Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui.

Soma Mithali 26