Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 12:11-14

Methali 12:11-14 BHN

Mkulima mwenye bidii ana chakula tele, lakini afuataye mambo yasiyofaa hana akili. Waovu hutamani faida isiyo halali, lakini mtu mwadilifu husimama imara. Mtu mwovu hunaswa kwa uongo wake mwenyewe, lakini mwadilifu hutoka katika taabu. Mtu hufanikiwa kutokana na maneno yake kama apatavyo matokeo ya kazi za mikono yake.

Soma Methali 12