Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 27:57-60

Mathayo 27:57-60 BHN

Ilipokuwa jioni, akaja mtu mmoja tajiri mwenyeji wa Arimathaya, jina lake Yosefu. Yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. Akamwendea Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. Basi, Pilato akaamuru apewe. Yosefu akauchukua ule mwili, akauzungushia sanda safi ya kitani, akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mathayo 27:57-60