Luka 13:18-21
Luka 13:18-21 BHN
Yesu akauliza: “Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Nitaulinganisha na nini? Ni kama mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake; ikaota na kuwa mti. Ndege wa angani wakajenga viota vyao katika matawi yake.” Tena akauliza: “Nitaulinganisha ufalme wa Mungu na nini? Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na unga madebe mawili na nusu kisha unga wote ukaumuka.”