Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 13:18-21

Luka 13:18-21 BHN

Yesu akauliza: “Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Nitaulinganisha na nini? Ni kama mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake; ikaota na kuwa mti. Ndege wa angani wakajenga viota vyao katika matawi yake.” Tena akauliza: “Nitaulinganisha ufalme wa Mungu na nini? Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na unga madebe mawili na nusu kisha unga wote ukaumuka.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Luka 13:18-21