Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 11:5-10

Luka 11:5-10 BHN

Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu anaye rafiki, akaenda kwake usiku wa manane, akamwambia: ‘Rafiki, tafadhali niazime mikate mitatu, kwa kuwa rafiki yangu amepitia kwangu akiwa safarini nami sina cha kumpa.’ Naye, akiwa ndani angemjibu: ‘Usinisumbue! Nimekwisha funga mlango. Mimi na watoto wangu tumelala; siwezi kuamka nikupe!’ Hakika, ingawa hataamka ampe kwa sababu yeye ni rafiki yake, lakini, kwa sababu ya huyo mtu kuendelea kumwomba, ataamka ampe chochote anachohitaji. Kwa hiyo, ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni mlango nanyi mtafunguliwa. Maana yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata na abishaye mlango hufunguliwa.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Luka 11:5-10

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha