Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 11:5-10

Luka 11:5-10 SRUV

Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu, kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake; na yule wa ndani amjibu akisema, Usinisumbue; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kutoka nikupe? Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa hatoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, atatoka na kumpa kadiri ya haja yake. Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

Soma Luka 11

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Luka 11:5-10