Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 40:6-14

Yobu 40:6-14 BHN

Hapo Mwenyezi-Mungu akamjibu kutoka kimbunga: “Jikaze kama mwanamume. Nitakuuliza, nawe utanijibu. Je, unataka kweli kubatilisha hukumu yangu, kuniona nina hatia ili wewe usiwe na hatia? Je, una nguvu kama mimi Mungu? Waweza kunguruma kwa sauti kama yangu? “Basi, jioneshe kuwa na fahari na ukuu, ujipambe kwa utukufu na fahari. Wamwagie watu hasira yako kuu; mwangalie kila mwenye kiburi na kumwangusha. Mwangalie kila mwenye kiburi na kumporomosha, uwakanyage waovu mahali walipo. Wazike wote pamoja ardhini; mfunge kila mmoja kwa kifungo cha kifo. Hapo nitakutambua, kwamba nguvu yako mwenyewe imekupa ushindi.

Soma Yobu 40