Yobu 40:6-14
Yobu 40:6-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Jifunge viuno kama mwanamume, Mimi nitakuuliza neno, nawe niambie. Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki? Au je! Wewe una mkono kama Mungu? Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye? Haya! Jivike sasa fahari na ukuu; Jipambe heshima na enzi. Mwaga mafuriko ya hasira zako, Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhili. Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe, Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo. Wafiche mavumbini pamoja, Wafunge nyuso zao mahali palipositirika. Ndipo mimi nami nitazikiri habari zako, Ya kuwa mkono wako wa kuume waweza kukuokoa.
Yobu 40:6-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Hapo Mwenyezi-Mungu akamjibu kutoka kimbunga: “Jikaze kama mwanamume. Nitakuuliza, nawe utanijibu. Je, unataka kweli kubatilisha hukumu yangu, kuniona nina hatia ili wewe usiwe na hatia? Je, una nguvu kama mimi Mungu? Waweza kunguruma kwa sauti kama yangu? “Basi, jioneshe kuwa na fahari na ukuu, ujipambe kwa utukufu na fahari. Wamwagie watu hasira yako kuu; mwangalie kila mwenye kiburi na kumwangusha. Mwangalie kila mwenye kiburi na kumporomosha, uwakanyage waovu mahali walipo. Wazike wote pamoja ardhini; mfunge kila mmoja kwa kifungo cha kifo. Hapo nitakutambua, kwamba nguvu yako mwenyewe imekupa ushindi.
Yobu 40:6-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Jifunge viuno kama mwanamume, Mimi nitakuuliza neno, nawe niambie. Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki? Au je! Wewe una mkono kama Mungu? Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye? Haya! Jivike sasa fahari na ukuu; Jipambe heshima na enzi. Mwaga mafuriko ya hasira zako, Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhalilishe. Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe, Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo. Wafiche mavumbini pamoja, Wafunge nyuso zao mahali palipositirika. Ndipo mimi nami nitazikiri habari zako, Ya kuwa mkono wako wa kulia waweza kukuokoa.
Yobu 40:6-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo BWANA akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli: “Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu. “Je, utabatilisha hukumu yangu? Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe? Je, una mkono kama wa Mungu, nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake? Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari, nawe uvae heshima na enzi. Fungulia ukali wa ghadhabu yako, mtafute kila mwenye kiburi umshushe, mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze, waponde waovu mahali wasimamapo. Wazike wote mavumbini pamoja; wafunge nyuso zao kaburini. Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.