Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 40:6-14

Ayubu 40:6-14 NEN

Ndipo BWANA akasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli: “Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu. “Je, utabatilisha hukumu yangu? Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe? Je, una mkono kama wa Mungu, nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake? Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari, nawe uvae heshima na enzi. Fungulia ukali wa ghadhabu yako, mtafute kila mwenye kiburi umshushe, mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze, waponde waovu mahali wasimamapo. Wazike wote mavumbini pamoja; wafunge nyuso zao kaburini. Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.