Yobu 28:20-28
Yobu 28:20-28 BHN
“Basi, hekima yatoka wapi? Ni wapi panapopatikana maarifa? Imefichika machoni pa viumbe vyote hai, na ndege wa angani hawawezi kuiona. Abadoni na Kifo wasema, ‘Tumesikia uvumi wake kwa masikio yetu.’ “Mungu aijua njia ya hekima, anajua mahali inapopatikana. Maana yeye huona mpaka upeo wa dunia, huona kila kitu chini ya mbingu. Alipoupa upepo uzito wake, na kuyapimia maji mipaka yake; alipoamua mvua inyeshe wapi, umeme na radi vipite wapi; hapo ndipo alipoiona hekima na kuitangaza, aliisimika na kuichunguza.” Kisha Mungu akamwambia mwanadamu: “Tazama! Kumcha Bwana ndio hekima; na kujitenga na uovu ndio maarifa.”