Isaya 32:16-19
Isaya 32:16-19 BHN
Haki itadumu katika nchi iliyokuwa nyika, uadilifu utatawala katika mashamba yenye rutuba. Kutokana na uadilifu watu watapata amani, utulivu na usalama utadumu milele. Watu wangu watakaa katika makao ya amani, katika maskani salama na mazingira matulivu. Msitu wa adui utatoweka kabisa, na mji wake utaangamizwa.