Isaya 32:16-19
Isaya 32:16-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa katika shamba lizaalo sana. Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. Na watu wangu watakaa katika makao ya amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu. Lakini mvua ya mawe itanyesha, wakati wa kuangushwa miti ya msituni; na huo mji utadhilika.
Isaya 32:16-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Haki itadumu katika nchi iliyokuwa nyika, uadilifu utatawala katika mashamba yenye rutuba. Kutokana na uadilifu watu watapata amani, utulivu na usalama utadumu milele. Watu wangu watakaa katika makao ya amani, katika maskani salama na mazingira matulivu. Msitu wa adui utatoweka kabisa, na mji wake utaangamizwa.
Isaya 32:16-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa katika shamba lizaalo sana. Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. Na watu wangu watakaa katika kao la amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu. Lakini mvua ya mawe itakunya, wakati wa kuangushwa miti ya msituni; na huo mji utadhilika.
Isaya 32:16-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Haki itakaa katika jangwa, na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba. Matunda ya haki yatakuwa amani, matokeo ya haki yatakuwa utulivu na matumaini milele. Watu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani, katika nyumba zilizo salama, katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu. Hata kama mvua ya mawe iangushe msitu na mji ubomolewe kabisa