Isaya 32:16-19
Isaya 32:16-19 SRUV
Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa katika shamba lizaalo sana. Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. Na watu wangu watakaa katika makao ya amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu. Lakini mvua ya mawe itanyesha, wakati wa kuangushwa miti ya msituni; na huo mji utadhilika.