Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 3:8-11

Isaya 3:8-11 BHN

Watu wa Yerusalemu wamejikwaa, watu wa Yuda wameanguka, kwa kuwa wanampinga Mwenyezi-Mungu kwa maneno na matendo, wakipuuza utukufu wake miongoni mwao. Ubaguzi wao unashuhudia dhidi yao; wanatangaza dhambi yao kama ya Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao watu hao, kwani wamejiletea maangamizi wenyewe. Waambieni waadilifu jinsi walivyo na bahati: Kwani watakula matunda ya matendo yao. Lakini ole wao watu waovu! Mambo yatawaendea vibaya, kwani waliyotenda yatawapata wao wenyewe.

Soma Isaya 3