Isaya 3:8-11
Isaya 3:8-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha BWANA, hata wayachukize macho ya utukufu wake. Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu. Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa ijara ya mikono yake.
Isaya 3:8-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Watu wa Yerusalemu wamejikwaa, watu wa Yuda wameanguka, kwa kuwa wanampinga Mwenyezi-Mungu kwa maneno na matendo, wakipuuza utukufu wake miongoni mwao. Ubaguzi wao unashuhudia dhidi yao; wanatangaza dhambi yao kama ya Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao watu hao, kwani wamejiletea maangamizi wenyewe. Waambieni waadilifu jinsi walivyo na bahati: Kwani watakula matunda ya matendo yao. Lakini ole wao watu waovu! Mambo yatawaendea vibaya, kwani waliyotenda yatawapata wao wenyewe.

Isaya 3:8-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha BWANA, hata wakayachukiza macho ya utukufu wake. Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu. Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa malipo ya mikono yake.
Isaya 3:8-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha BWANA, hata wayachukize macho ya utukufu wake. Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu. Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa ijara ya mikono yake.
Isaya 3:8-11 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Yerusalemu inapepesuka, Yuda inaanguka; maneno yao na matendo yao ni kinyume na Mwenyezi Mungu, wakiudharau uwepo wake uliotukuka. Nyuso zao zinavyoonekana zinashuhudia dhidi yao, hujivunia dhambi yao kama Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao! Wamejiletea maafa juu yao wenyewe. Waambie wanyofu itakuwa heri kwao, kwa kuwa watafurahia tunda la matendo yao. Ole kwa watu waovu! Maafa yapo juu yao! Watalipwa kwa ajili ya yale mikono yao iliyotenda.