Isaya 3:8-11
Isaya 3:8-11 NENO
Yerusalemu inapepesuka, Yuda inaanguka; maneno yao na matendo yao ni kinyume na Mwenyezi Mungu, wakiudharau uwepo wake uliotukuka. Nyuso zao zinavyoonekana zinashuhudia dhidi yao, hujivunia dhambi yao kama Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao! Wamejiletea maafa juu yao wenyewe. Waambie wanyofu itakuwa heri kwao, kwa kuwa watafurahia tunda la matendo yao. Ole kwa watu waovu! Maafa yapo juu yao! Watalipwa kwa ajili ya yale mikono yao iliyotenda.