Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 3:8-11

Isaya 3:8-11 SRUV

Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha BWANA, hata wakayachukiza macho ya utukufu wake. Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu. Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa malipo ya mikono yake.

Soma Isaya 3