Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 7:17-24

Mwanzo 7:17-24 BHN

Gharika ilidumu nchini kwa muda wa siku arubaini. Maji yakaongezeka na kuiinua safina, ikaelea juu ya ardhi. Maji yakaendelea kuongezeka zaidi nchini na safina ikaelea juu yake. Maji hayo yakawa mengi sana juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu katika nchi. Yaliongezeka hata kuifunika milima kiasi cha mita saba na nusu. Viumbe wote hai katika nchi wakafa. Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama wa porini, makundi ya viumbe wote katika nchi kavu na wanadamu wote; naam, kila kiumbe hai katika nchi kavu kilikufa. Mungu akaangamiza kila kiumbe kilichokuwa hai duniani: Binadamu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Vyote viliangamizwa duniani. Noa tu ndiye aliyesalimika na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina. Maji hayo yalidumu katika nchi siku 150.

Soma Mwanzo 7