Mwanzo 7:17-24
Mwanzo 7:17-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Gharika ilidumu nchini kwa muda wa siku arubaini. Maji yakaongezeka na kuiinua safina, ikaelea juu ya ardhi. Maji yakaendelea kuongezeka zaidi nchini na safina ikaelea juu yake. Maji hayo yakawa mengi sana juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu katika nchi. Yaliongezeka hata kuifunika milima kiasi cha mita saba na nusu. Viumbe wote hai katika nchi wakafa. Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama wa porini, makundi ya viumbe wote katika nchi kavu na wanadamu wote; naam, kila kiumbe hai katika nchi kavu kilikufa. Mungu akaangamiza kila kiumbe kilichokuwa hai duniani: Binadamu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Vyote viliangamizwa duniani. Noa tu ndiye aliyesalimika na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina. Maji hayo yalidumu katika nchi siku 150.
Mwanzo 7:17-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arubaini; nayo maji yakazidi, yakaifanya safina ielee, ikaelea juu ya nchi. Maji yakaongezeka zaidi juu ya nchi; na safina ikaelea juu ya uso wa maji. Maji yakazidi kuongezeka sana sana juu ya nchi; hata milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikwa. Maji yakaongezeka hata milima ikafunikwa kiasi cha dhiraa kumi na tano. Wakafa watu wote waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu; kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu. Kila kilichokuwa hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali; mwanadamu, wanyama wa kufugwa, kitambaacho na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao waliokuwa pamoja naye katika safina. Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.

Mwanzo 7:17-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arobaini; nayo maji yakazidi, yakaieleza safina, ikaelea juu ya nchi. Maji yakapata nguvu, yakazidi sana juu ya nchi; na ile safina ikaelea juu ya uso wa maji. Maji yakapata nguvu sana sana juu ya nchi; na milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikizwa. Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano. Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu; kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu. Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina. Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.
Mwanzo 7:17-24 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani; maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka uso wa dunia. Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya dunia, na safina ikaelea juu ya maji. Maji yakazidi kujaa juu ya dunia, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote. Maji yakaendelea kujaa, yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano. Kila kiumbe hai kinachotambaa juu ya dunia kikaangamia: ndege, mifugo, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi, na wanadamu wote. Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa. Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali; watu, wanyama pori, viumbe vinavyotambaa ardhini, na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Nuhu peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina. Maji yakaifunika dunia kwa siku mia moja na hamsini.