Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 7:17-24

Mwanzo 7:17-24 SRUV

Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arubaini; nayo maji yakazidi, yakaifanya safina ielee, ikaelea juu ya nchi. Maji yakaongezeka zaidi juu ya nchi; na safina ikaelea juu ya uso wa maji. Maji yakazidi kuongezeka sana sana juu ya nchi; hata milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikwa. Maji yakaongezeka hata milima ikafunikwa kiasi cha dhiraa kumi na tano. Wakafa watu wote waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu; kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu. Kila kilichokuwa hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali; mwanadamu, wanyama wa kufugwa, kitambaacho na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao waliokuwa pamoja naye katika safina. Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.

Soma Mwanzo 7