Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 49:13-27

Mwanzo 49:13-27 BHN

“Zebuluni ataishi sehemu za pwani, pwani yake itakuwa mahali pa kuegesha meli. Nchi yake itapakana na Sidoni. “Isakari ni kama punda mwenye nguvu, ajilazaye kati ya mizigo yake. “Aliona kuwa mahali pa kupumzikia ni pema, na kwamba nchi ni ya kupendeza, akauinamisha mgongo wake kubeba mzigo, akawa mtumwa kufanya kazi za shuruti. “Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake, kama mojawapo ya makabila ya Israeli. “Atakuwa kama nyoka njiani, nyoka mwenye sumu kando ya njia, aumaye visigino vya farasi, naye mpandafarasi huanguka chali. “Ee Mwenyezi-Mungu, nangojea uniokoe! “Gadi atashambuliwa na wanyanganyi, lakini yeye atawafuata nyuma na kuwashambulia. “Ardhi ya Asheri itatoa mavuno kwa wingi, naye atatoa chakula kimfaacho mfalme. “Naftali ni kama paa aliye huru, azaaye watoto walio wazuri. “Yosefu ni kama mti uzaao, mti uzaao kando ya chemchemi, matawi yake hutanda ukutani. “Wapiga mishale walimshambulia vikali, wakamtupia mishale na kumsumbua sana. “Lakini upinde wake bado imara, na mikono yake imepewa nguvu, kwa uwezo wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli; “kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia, kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki; upate baraka za mvua toka juu mbinguni, baraka za maji ya vilindi vilivyo chini, baraka za uzazi wa akina mama na mifugo. Baraka za baba yako zishinde baraka za milima ya milele, ziwe bora kuliko vilima vya kale. Baraka hizo na ziwe juu ya kichwa cha Yosefu, juu ya paji lake yeye aliyekuwa ametengwa na ndugu zake. “Benyamini ni mbwamwitu mkali; asubuhi hula mawindo yake, na jioni hugawa nyara.”

Soma Mwanzo 49

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwanzo 49:13-27