Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwa 49:13-27

Mwa 49:13-27 SUV

Zabuloni atakaa pwani ya bahari, Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu, Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni. Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo; Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu. Dani atahukumu watu wake, Kama moja ya makabila ya Israeli; Dani atakuwa nyoka barabarani, Bafe katika njia, Aumaye visigino vya farasi, Hata apandaye ataanguka chali. Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA. Gadi, jeshi litamsonga, Lakini atawasonga wao mpaka visigino. Asheri, chakula chake kitakuwa kinono, Naye atatoa tunu za kifalme. Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri. Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matwi yake yametanda ukutani. Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi, Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli, Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba. Mibaraka ya baba yako Imepita mibaraka ya milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake. Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye kurarua-rarua Asubuhi atakula mawindo, Na jioni atagawanya mateka.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwa 49:13-27