Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 20:22-26

Kutoka 20:22-26 BHN

Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli: ‘Mmejionea nyinyi wenyewe kwamba nimeongea nanyi kutoka mbinguni. Mtaniheshimu mimi peke yangu wala msijifanyie miungu ya fedha wala ya dhahabu. Nyinyi mtanijengea madhabahu ya udongo ambayo juu yake mtanitambikia kondoo wenu na ng'ombe wenu kama sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Mahali popote nitakapowakumbusha watu jina langu, papo hapo mimi mwenyewe nitawajia na kuwabariki. Kama mkinijengea madhabahu ya mawe, msiitengeneze kwa mawe ya kuchonga, maana mkitumia vyombo vya kuchongea mawe, mtaitia najisi. Wala msitengeneze madhabahu yenye ngazi za kupandia, mtu asije akauona uchi wa huyo anayepanda juu yake.’

Soma Kutoka 20

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kutoka 20:22-26