Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 20:22-26

Kutoka 20:22-26 SRUV

BWANA akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli hivi, Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni. Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie. Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo wako, na ng'ombe wako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia. Nawe ukinifanyia madhabahu ya mawe, hutaijenga ya mawe yaliyochongwa; kwa kuwa ukiwa umetumia chombo chako katika kuichonga umeitia unajisi. Tena hutapanda kwenda madhabahuni kwangu kwa daraja, uchi wako usidhihirike juu yake.

Soma Kutoka 20

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kutoka 20:22-26