Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 20

20
Amri kumi
(Kumb 5:1-21)
1Mwenyezi-Mungu alizungumza maneno haya yote, akasema, 2“Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, niliyekutoa nchini Misri, ambako ulikuwa mtumwa.
3“Usiwe na miungu mingine ila mimi.#20:3 Usiwe … mimi: Au usiwe na miungu mingine zaidi yangu.
4 # Taz Kut 34:17; Lawi 19:4; 26:1; Kumb 4:15-18; 27:15 “Usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago cha chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia. 5#Taz Kut 34:6-7; Hes 14:18; Kumb 7:9-10 Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao. 6Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.
7 # Taz Lawi 19:12; Kumb 18:20; Roma 13:9; Yak 2:11 “Usilitaje bure jina langu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Maana mimi Mwenyezi-Mungu sitaacha kumwadhibu anayetumia jina langu vibaya.
8“Usisahau kuiweka takatifu siku ya Sabato. 9Siku sita fanya kazi na tenda mambo yako yote. 10Lakini siku ya saba ni Sabato ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala watumishi wako wa kike, wala mnyama wako wa kufugwa, wala mgeni aliye nyumbani mwako. 11Maana kwa siku sita mimi Mwenyezi-Mungu niliziumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo, kisha nikapumzika siku ya saba. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu niliibariki siku ya Sabato, nikaitakasa.
12“Waheshimu baba yako na mama yako, ili uishi maisha marefu katika nchi ninayokupa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.
13“Usiue.
14“Usizini.
15 # Taz Lawi 19:11; Mat 19:18; Marko 10:19; Luka 18:20; Roma 13:9 “Usiibe.
16 # Taz Kut 23:1 Mat 19:18; Marko 10:19; Luka 18:20 “Usimshuhudie jirani yako uongo.
17“Usiitamani nyumba ya jirani yako, wala mke wake, wala mtumwa wake wa kiume au wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala chochote kilicho mali ya jirani yako.”
18Watu waliposikia ngurumo na kuona umeme ukiwaka na kuisikia sauti ya parapanda juu ya mlima uliokuwa unafuka moshi, wote waliogopa na kutetemeka. Wote walisimama mbali, 19wakamwambia Mose, “Ongea nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza, lakini Mwenyezi-Mungu asiongee nasi, tusije tukafa.” 20Mose akawaambia, “Msiogope, maana Mungu amekuja kuwajaribu ili mpate kumcha yeye daima na msitende dhambi.”
21Watu wote walisimama mbali wakati Mose alipokaribia lile wingu zito alimokuwamo Mungu.
Sheria kuhusu madhabahu
22Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli: ‘Mmejionea nyinyi wenyewe kwamba nimeongea nanyi kutoka mbinguni. 23Mtaniheshimu mimi peke yangu wala msijifanyie miungu ya fedha wala ya dhahabu. 24Nyinyi mtanijengea madhabahu ya udongo ambayo juu yake mtanitambikia kondoo wenu na ng'ombe wenu kama sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Mahali popote nitakapowakumbusha watu jina langu, papo hapo mimi mwenyewe nitawajia na kuwabariki. 25#Taz Kumb 27:5-7; Yosh 8:31 Kama mkinijengea madhabahu ya mawe, msiitengeneze kwa mawe ya kuchonga, maana mkitumia vyombo vya kuchongea mawe, mtaitia najisi. 26Wala msitengeneze madhabahu yenye ngazi za kupandia, mtu asije akauona uchi wa huyo anayepanda juu yake.’

Iliyochaguliwa sasa

Kutoka 20: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha