Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 1:1-27

1 Mambo ya Nyakati 1:1-27 BHN

Adamu alimzaa Sethi, Sethi akamzaa Enoshi, Enoshi akamzaa Kenani, Kenani akamzaa Mahalaleli, Mahalaleli akamzaa Yaredi, Yaredi akamzaa Henoki, Henoki akamzaa Methusela. Methusela alimzaa Lameki, Lameki akamzaa Noa. Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi. Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Difathi na Togama. Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani. Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani. Kushi alimzaa Nimrodi, aliyekuwa mtu shujaa wa kwanza duniani. Wazawa wa Misri ni Waludi, Waanamu, Walehabi, Wanaftuhi, Wapathrusi Wakaftori na Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti). Wana wa Kanaani walikuwa Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi. Kanaani pia ndiye babu yao Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waarki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuri, Arpaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri na Mesheki. Arpaksadi alimzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. Eberi alikuwa na wana wawili; mmoja wao aliitwa Pelegi, (kwa maana wakati wake watu walikuwa wametawanyika duniani), na ndugu yake aliitwa Yoktani. Wana wa Yoktani walikuwa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Havila na Yobabu. Hao watu ni wana wa Yoktani. Ukoo wa Abrahamu kutokea Shemu ni kama ifuatavyo: Shemu alimzaa Arpaksadi, naye Arpaksadi akamzaa Shela. Shela akamzaa Eberi, Eberi akamzaa Pelegi, Pelegi akamzaa Reu; Reu akamzaa Serugi, Serugi akamzaa Nahori, Nahori akamzaa Tera, na Tera akamzaa Abramu, ambaye ndiye Abrahamu.