Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati 1:1-27

1 Nyakati 1:1-27 NEN

Adamu, Sethi, Enoshi, Kenani, Mahalaleli, Yaredi, Enoki, Methusela, Lameki, Noa. Wana wa Noa walikuwa: Shemu, Hamu na Yafethi. Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma. Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani. Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani. Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi. Misraimu akawazaa: Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori. Wana wa Kanaani walikuwa: Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waariki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki. Arfaksadi akamzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. Eberi alipata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani. Wana wa Yoktani walikuwa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani. Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela, Eberi, Pelegi, Reu, Serugi, Nahori, Tera, Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu).